sw_tn/gal/04/24.md

28 lines
1.0 KiB
Markdown

# Sentensi unganishi
Paulo anaanza habari kwa kueleza ukweli kuwa neema na sheria haziwezi kuwa sehemu moja kwa pamoja na kwa wakati mmoja.
# Mambo haya yanaweza kuelezwa kwa kutumia mfano,
"Habari hii ya wana wawili ni picha hii ya kile ninachowambieni sasa."
# mfano
Mfano ni namna ya kiuandishi uliotumika kutoa maana fulani, mfano; watu na vitu vimetumika kuwakilisha vitu vingine au maana fulani. Katika mfano huu wa Paulo, wanawake wawili wametumika kurejelea aina mbili za maagano 4:21.
# Mlima Sinai
Mlima Sinai umetumika kama kiwakilishi cha sheria. Ni mahali Musa alipopokea mbao mbili za sheria kwa ajili ya wana wa Waisrael.
# Huzaa watoto ambao ni watumwa
Paulo anaiona sheria kama vile ni mtu. Watu waliochini ya agano la sheria ni watumwa wanaopaswa kuitii sheria.
# Fananishwa
Ni mifano yenye kutoa picha ya kuleta maana fulani.
# Yuko katika utumwa pamoja na watoto wake
Hajiri ni mtumwa na watoto wake wako utumwani pamoja naye. Yerusalemu ni kama Hajiri na watoto wake ni watumwa pamoja naye.