sw_tn/gal/04/24.md

1.0 KiB

Sentensi unganishi

Paulo anaanza habari kwa kueleza ukweli kuwa neema na sheria haziwezi kuwa sehemu moja kwa pamoja na kwa wakati mmoja.

Mambo haya yanaweza kuelezwa kwa kutumia mfano,

"Habari hii ya wana wawili ni picha hii ya kile ninachowambieni sasa."

mfano

Mfano ni namna ya kiuandishi uliotumika kutoa maana fulani, mfano; watu na vitu vimetumika kuwakilisha vitu vingine au maana fulani. Katika mfano huu wa Paulo, wanawake wawili wametumika kurejelea aina mbili za maagano 4:21.

Mlima Sinai

Mlima Sinai umetumika kama kiwakilishi cha sheria. Ni mahali Musa alipopokea mbao mbili za sheria kwa ajili ya wana wa Waisrael.

Huzaa watoto ambao ni watumwa

Paulo anaiona sheria kama vile ni mtu. Watu waliochini ya agano la sheria ni watumwa wanaopaswa kuitii sheria.

Fananishwa

Ni mifano yenye kutoa picha ya kuleta maana fulani.

Yuko katika utumwa pamoja na watoto wake

Hajiri ni mtumwa na watoto wake wako utumwani pamoja naye. Yerusalemu ni kama Hajiri na watoto wake ni watumwa pamoja naye.