# Sentensi unganishi Paulo anaanza habari kwa kueleza ukweli kuwa neema na sheria haziwezi kuwa sehemu moja kwa pamoja na kwa wakati mmoja. # Mambo haya yanaweza kuelezwa kwa kutumia mfano, "Habari hii ya wana wawili ni picha hii ya kile ninachowambieni sasa." # mfano Mfano ni namna ya kiuandishi uliotumika kutoa maana fulani, mfano; watu na vitu vimetumika kuwakilisha vitu vingine au maana fulani. Katika mfano huu wa Paulo, wanawake wawili wametumika kurejelea aina mbili za maagano 4:21. # Mlima Sinai Mlima Sinai umetumika kama kiwakilishi cha sheria. Ni mahali Musa alipopokea mbao mbili za sheria kwa ajili ya wana wa Waisrael. # Huzaa watoto ambao ni watumwa Paulo anaiona sheria kama vile ni mtu. Watu waliochini ya agano la sheria ni watumwa wanaopaswa kuitii sheria. # Fananishwa Ni mifano yenye kutoa picha ya kuleta maana fulani. # Yuko katika utumwa pamoja na watoto wake Hajiri ni mtumwa na watoto wake wako utumwani pamoja naye. Yerusalemu ni kama Hajiri na watoto wake ni watumwa pamoja naye.