sw_tn/gal/04/12.md

798 B

Sentensi unganishi

Paulo anawakumbusha waumini wa Galatia jinsi walivyokuwa wema katkia kumhudumia wakati akiwa pamoja nao, na anawatia moyo kuendelea kumtumaini hata wakati asipokuwa pamoja nao.

Sihi

Neno hili linamaanisha kuomba kwa nguvu. Hili si neno lililotumika kuomba pesa, chakula au kitu kingine chochote cha mahitaji.

Ndugu

Hapa linamaanisha wakristo wote wa kike na wakiume, ndugu walio katika Kristo ni washirika wa familia moja ya kiroho, pamoja na Mungu Baba yao wa mbinguni.

Hamjanitenda kosa

kwa kutumia maneno haya, Paulo anatilia mkazo kwa Wagalatia walihudumia vizuri sana "Mlinitunza vizuri sana", au "mlinitunza kama mlivyopaswa"

Ingawa afya yangu iliwaweka katika jaribu

"Ingawa ilikuwa vigumu kuniona mimi wakati nikiwa mgonjwa"

kudharau

kuchukia sana