# Sentensi unganishi Paulo anawakumbusha waumini wa Galatia jinsi walivyokuwa wema katkia kumhudumia wakati akiwa pamoja nao, na anawatia moyo kuendelea kumtumaini hata wakati asipokuwa pamoja nao. # Sihi Neno hili linamaanisha kuomba kwa nguvu. Hili si neno lililotumika kuomba pesa, chakula au kitu kingine chochote cha mahitaji. # Ndugu Hapa linamaanisha wakristo wote wa kike na wakiume, ndugu walio katika Kristo ni washirika wa familia moja ya kiroho, pamoja na Mungu Baba yao wa mbinguni. # Hamjanitenda kosa kwa kutumia maneno haya, Paulo anatilia mkazo kwa Wagalatia walihudumia vizuri sana "Mlinitunza vizuri sana", au "mlinitunza kama mlivyopaswa" # Ingawa afya yangu iliwaweka katika jaribu "Ingawa ilikuwa vigumu kuniona mimi wakati nikiwa mgonjwa" # kudharau kuchukia sana