sw_tn/gal/03/06.md

28 lines
1.1 KiB
Markdown

# Sentensi unganishi:
Paulo anawakumbusha Waumini wa Galatia kwamba hata Ibrahimu aliipokea haki kwa imani na siyo kwa sheria.
# ilihesabiwa kwake mwenye haki
Mungu aliiona imani ya Ibrahimu katika Mungu, hivyo Mungu alimhesabia Ibrahimu haki.
# ambao wanaamini ( wenye imani)
"watu walioamini" Maana ya nomino 'imani' laweza kuelezwa kwa kitenzi 'kuamini" "wale wanaoamini"
# watoto wa Ibrahimu
inawakilisha watu wale ambao Mungu huwatazama kama alivyomtazama Ibrahimu. "Mwenye haki kwa namna moja kama ya Ibrahimu."
# tangulia kuwaona
Kwa sababu Mungu alimwahidi Ibrahimu na ikaandikwa kabla ahadi hiyo kuja kupitia Kristo, maandiko ni kama mtu ambaye huona muda ujao kabla ya kutokea. "Ilitabiriwa" au " kuona kitu kabla hakijatokea."
# katika wewe
"Kwa sababu ya kile umekwisha tenda" au "kwasababu nimekwisha kukubariki" Neno wewe humrejelea Ibrahimu katika umoja.
# mataifa yote
"makundi ya watu wote duniani". Mungu alikuwa akielezea kwa mkazo kwamba alikuwa hapendelei wayahudi tu, kundi alilolichagua. Mpango wake wa wokovu ulikuwa kwa wote wayahudu na wasio wayahudi.