# Sentensi unganishi: Paulo anawakumbusha Waumini wa Galatia kwamba hata Ibrahimu aliipokea haki kwa imani na siyo kwa sheria. # ilihesabiwa kwake mwenye haki Mungu aliiona imani ya Ibrahimu katika Mungu, hivyo Mungu alimhesabia Ibrahimu haki. # ambao wanaamini ( wenye imani) "watu walioamini" Maana ya nomino 'imani' laweza kuelezwa kwa kitenzi 'kuamini" "wale wanaoamini" # watoto wa Ibrahimu inawakilisha watu wale ambao Mungu huwatazama kama alivyomtazama Ibrahimu. "Mwenye haki kwa namna moja kama ya Ibrahimu." # tangulia kuwaona Kwa sababu Mungu alimwahidi Ibrahimu na ikaandikwa kabla ahadi hiyo kuja kupitia Kristo, maandiko ni kama mtu ambaye huona muda ujao kabla ya kutokea. "Ilitabiriwa" au " kuona kitu kabla hakijatokea." # katika wewe "Kwa sababu ya kile umekwisha tenda" au "kwasababu nimekwisha kukubariki" Neno wewe humrejelea Ibrahimu katika umoja. # mataifa yote "makundi ya watu wote duniani". Mungu alikuwa akielezea kwa mkazo kwamba alikuwa hapendelei wayahudi tu, kundi alilolichagua. Mpango wake wa wokovu ulikuwa kwa wote wayahudu na wasio wayahudi.