sw_tn/gal/03/06.md

1.1 KiB

Sentensi unganishi:

Paulo anawakumbusha Waumini wa Galatia kwamba hata Ibrahimu aliipokea haki kwa imani na siyo kwa sheria.

ilihesabiwa kwake mwenye haki

Mungu aliiona imani ya Ibrahimu katika Mungu, hivyo Mungu alimhesabia Ibrahimu haki.

ambao wanaamini ( wenye imani)

"watu walioamini" Maana ya nomino 'imani' laweza kuelezwa kwa kitenzi 'kuamini" "wale wanaoamini"

watoto wa Ibrahimu

inawakilisha watu wale ambao Mungu huwatazama kama alivyomtazama Ibrahimu. "Mwenye haki kwa namna moja kama ya Ibrahimu."

tangulia kuwaona

Kwa sababu Mungu alimwahidi Ibrahimu na ikaandikwa kabla ahadi hiyo kuja kupitia Kristo, maandiko ni kama mtu ambaye huona muda ujao kabla ya kutokea. "Ilitabiriwa" au " kuona kitu kabla hakijatokea."

katika wewe

"Kwa sababu ya kile umekwisha tenda" au "kwasababu nimekwisha kukubariki" Neno wewe humrejelea Ibrahimu katika umoja.

mataifa yote

"makundi ya watu wote duniani". Mungu alikuwa akielezea kwa mkazo kwamba alikuwa hapendelei wayahudi tu, kundi alilolichagua. Mpango wake wa wokovu ulikuwa kwa wote wayahudu na wasio wayahudi.