sw_tn/gal/01/15.md

878 B

Aliniita kupitia neema yake

Maana zinazokubalika ni 1)"Mungu aliniita kumtumikia kwa sababu Yeye ni wa neema" au 2) " Aliniita kwa njia ya neema yake."

kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu

Maana zinazokubalika 1)" kuniruhusu mimi nimjue Mwana wake" 2) "Ulimwengu umwone Yesu Mwana wa Mungu kupitia kwangu."

Mwana

Hili ni jina muhimu la Yesu, Mwana wa Mungu

kumtangaza Yeye

Kumtangaza kuwa Yeye ni Mwana wa Mungu" au "kuhubiri habari njema kuhusu Mwana wa Mungu"

Wala sikutafuta ushauri wa mwili na damu

Haya maelezo yanamaanisha kuzungumza na watu wengine. AT: " kuwaomba watu wanisaidie kuelewa ujumbe."

kupanda

AT: "Kusafiri" Mji wa Yerusalem ulikuwa katika mkoa ulikuwa na milima mingi, ambayo ilimlazimu mtu kupanda milima mingi ili kufika huko, na hivyo ilikuwa kawaida kueleza kitendo cha kusafiri kwenda Yerusalemu kama "kupanda kwenda Yerusalemu."