sw_tn/ezk/30/04.md

40 lines
1.0 KiB
Markdown

# Maelezo ya Jumla:
Haya ni maneno ya Yahwe kuhusu Misri
# Kisha upanga utakuja juu ya Misri
Neno "upanga" hapa linarejea kwa vita au shambulizi. "Kutakuwa na vita juu ya Misri"
# kutakuwa na maumivu makali katika Kushi
"Kushi itakuwa na huzuni sana" au "watu wa Kushi watakuwa na huzuni kubwa sana"
# wakati wauaji wa watu watakapoanguka katika Misri
"wakati watu wa Misri watakapouawa" au "wakati watu wengi katika Misri watakapokufa katika vita."
# wakati watakapochukua utajiri wake
"Washambuliaji watauchukua utajiri wa misri"
# wakati msingi wake utakapoharibiwa
"Washambuliaji wataiharibu hata misingi ya majengo katika Misri"
# Libya
Libya ni nchi ya magharibi mwa Misri.
# Ludi
Hii ni kama inaurejea ufalme wa Ludi ambayo kwa sasa ni Uturuki. Ezekieli anaiita mkoa wa Ludi.
# watu wa nyumba ya agano
"Wayahudi wanaoishi Misri"
# wataanguka kwa upanga
"watakufa kwa mapambano" au "watakufa kwa upanga." Hii haimaanishi kwamba kila mtu atakufa, lakini kwamba watu wengi kutoka hizi nchi zote watakufa.