sw_tn/exo/15/06.md

28 lines
902 B
Markdown

# Mkono wako wakulia, Yahweh, una nguvu ya utukufu
Musa anamzungumzia Mungu kama Mungu ana mikono. Mkono wa kulia wa husu nguvu ya Mungu au vitu Mungu anavyo fanya kwa nguvu.
# mkono wako, Yahweh, umewavunja adui
Musa anamzungumzia Mungu kama Mungu ana mikono. Mkono wa kulia wa husu nguvu ya Mungu.
# umewavunja adui
Musa anazungumzia adui kana kwamba ni dhahifu na waweza vunjwa kama kio au chungu.
# walio inuka dhidi yako
Kuasi dhidi ya Mungu kuna zungumziwa kama kujiinua dhidi yake.
# Umetuma gadhabu
Musa anazungumzia gadhabu ya Mungu kana kwamba ni mtumishi aliye mtuma kufanya kitu
# imewateketeza kama karatasi
Musa anazungumzia gadhabu ya Mungu kana kwamba ni moto unao weza kuchoma vitu. Maadui zake waliharibiwa kabisa kama karatasi.
# Kwa pumzi ya pua yako
Musa anamzungumzia Mungu kana kwamba Mungu ana pua, na upepo kana kwamba Mungu kapuliza upepo kwa kutoka puani mwake.