sw_tn/eph/05/08.md

799 B

Hapo kale ulikuwa giza

Kama tu mmoja hawezi kuona gizani, ndivyo watu wanaoishi katika dhambi wanapungukiwa ufahamu wa kiroho.

Lakini sasa ninyi ni nuru katika Bwana

Kama tu mmoja anaweza kuona katika nuru, ndivyo watu ambao wanaishi katika haki wanaufahamu wa kiroho.

kwa sababu tunda la haki ni uzuri wote, haki, na kweli

kazi zinazotoka kwenye maisha ya muumini (uzuri, haki, na kweli) zinafanana na tunda zuri linalozalishwa na mti wenye afya.

hazina ushirikiano pamoja na kazi zisizozaa za giza

"Usijihusishe na kazi za dhambi au wasioamini"

kazi zisizozaa za giza

kazi za mtu fulani anayeishi katika giza la kiroho zinafanana na matendo maovu ya watu wanaofanya kazi za uovu wamefichwa na giza usiku.

lakini afadhali uwafichue

"lakini heri uwaweke wazi kuwa wanamakosa"