sw_tn/eph/04/20.md

24 lines
976 B
Markdown

# Lakini hivi sivyo mlivyojifunza kuhusu Kristo
"Lakini hamkujifunza kumfuata Kristo kwa namna hii"
# Kama mmesikia kuhusu yeye na mmefundishwa katika yeye, kama ilivyo kweli iliyo ndani ya Yesu
"Kwavile mmesikia kuhusu Yesu na mmejifunza ukweli kuhusu yeye"
# Ninyi lazima mvue utu wa kale- ule ambao unakubaliana na tabia zenu za kale, ambao umeharibika sawasawa na tamaa za udanganyifu
AT: "Ninyi lazima mziondoe tabia ambazo zilikuwa za kawaida kwa njia za maisha yenu ya kale, ambazo zilikuwa mbaya kama tamaa zenu mbaya zilivyowadanganya ninyi"
# Lazima muuvue utu wa kale
Lazima mwachane na tabia zote za dhambi kama tu kuvua nguo na kuzitupa mbali. AT: "Lazima mbadili tabia zenu."
# Zile zinazoendana na mwenendo wenu wa kale
AT: "tabia ambazo zinakubaliana na asili yenu ya kale" au "tabia ambazo zinakubaliana na ukale wenu"
# Ambayo imeharibiwa kulingana na tamaa danganyifu
AT: "ambayo inaendelea kukua vibaya kwasababu ya tamaa za mwili zidanganyazo"