# Lakini hivi sivyo mlivyojifunza kuhusu Kristo "Lakini hamkujifunza kumfuata Kristo kwa namna hii" # Kama mmesikia kuhusu yeye na mmefundishwa katika yeye, kama ilivyo kweli iliyo ndani ya Yesu "Kwavile mmesikia kuhusu Yesu na mmejifunza ukweli kuhusu yeye" # Ninyi lazima mvue utu wa kale- ule ambao unakubaliana na tabia zenu za kale, ambao umeharibika sawasawa na tamaa za udanganyifu AT: "Ninyi lazima mziondoe tabia ambazo zilikuwa za kawaida kwa njia za maisha yenu ya kale, ambazo zilikuwa mbaya kama tamaa zenu mbaya zilivyowadanganya ninyi" # Lazima muuvue utu wa kale Lazima mwachane na tabia zote za dhambi kama tu kuvua nguo na kuzitupa mbali. AT: "Lazima mbadili tabia zenu." # Zile zinazoendana na mwenendo wenu wa kale AT: "tabia ambazo zinakubaliana na asili yenu ya kale" au "tabia ambazo zinakubaliana na ukale wenu" # Ambayo imeharibiwa kulingana na tamaa danganyifu AT: "ambayo inaendelea kukua vibaya kwasababu ya tamaa za mwili zidanganyazo"