sw_tn/eph/04/20.md

976 B

Lakini hivi sivyo mlivyojifunza kuhusu Kristo

"Lakini hamkujifunza kumfuata Kristo kwa namna hii"

Kama mmesikia kuhusu yeye na mmefundishwa katika yeye, kama ilivyo kweli iliyo ndani ya Yesu

"Kwavile mmesikia kuhusu Yesu na mmejifunza ukweli kuhusu yeye"

Ninyi lazima mvue utu wa kale- ule ambao unakubaliana na tabia zenu za kale, ambao umeharibika sawasawa na tamaa za udanganyifu

AT: "Ninyi lazima mziondoe tabia ambazo zilikuwa za kawaida kwa njia za maisha yenu ya kale, ambazo zilikuwa mbaya kama tamaa zenu mbaya zilivyowadanganya ninyi"

Lazima muuvue utu wa kale

Lazima mwachane na tabia zote za dhambi kama tu kuvua nguo na kuzitupa mbali. AT: "Lazima mbadili tabia zenu."

Zile zinazoendana na mwenendo wenu wa kale

AT: "tabia ambazo zinakubaliana na asili yenu ya kale" au "tabia ambazo zinakubaliana na ukale wenu"

Ambayo imeharibiwa kulingana na tamaa danganyifu

AT: "ambayo inaendelea kukua vibaya kwasababu ya tamaa za mwili zidanganyazo"