sw_tn/eph/02/11.md

28 lines
748 B
Markdown

# Maelezo au Sentensi unganishi:
Paulo anawakumbusha hawa waamini kwamba Mungu aliwafanya watu wamataifa na Wayahudi kuwa mwili mmoja kupitia Kristo na msalaba wake.
# wamataifa kwa jinsi ya mwili
Hii inaongelea juu watu ambao hawakuzaliwa Wayahudi.
# msiyotairiwa
Watu ambao si Wayahudi hawakutairiwa walipokuwa watoto na hivyo Wayahudi waliwaona hao kama watu wasiomfuata Mungu.
# tohara
Hili lilikuwa neno lingine linaloelezea juu ya Wayahudi kwa sababu watoto wote wachanga wa kiume walitairiwa walipokuwa na umri wa siku nane.
# tohara ya mwili
Kutahiriwa kulifanywa juu ya miili ya watoto wadogo wa kiume.
# watu wa Israel
"jamii ya watu wa Israel"
# wageni kwa agano la ahadi
Tafsiri mbadala: "hamkujua ahadi za agano la Mungu"