sw_tn/eph/02/11.md

748 B

Maelezo au Sentensi unganishi:

Paulo anawakumbusha hawa waamini kwamba Mungu aliwafanya watu wamataifa na Wayahudi kuwa mwili mmoja kupitia Kristo na msalaba wake.

wamataifa kwa jinsi ya mwili

Hii inaongelea juu watu ambao hawakuzaliwa Wayahudi.

msiyotairiwa

Watu ambao si Wayahudi hawakutairiwa walipokuwa watoto na hivyo Wayahudi waliwaona hao kama watu wasiomfuata Mungu.

tohara

Hili lilikuwa neno lingine linaloelezea juu ya Wayahudi kwa sababu watoto wote wachanga wa kiume walitairiwa walipokuwa na umri wa siku nane.

tohara ya mwili

Kutahiriwa kulifanywa juu ya miili ya watoto wadogo wa kiume.

watu wa Israel

"jamii ya watu wa Israel"

wageni kwa agano la ahadi

Tafsiri mbadala: "hamkujua ahadi za agano la Mungu"