# Maelezo au Sentensi unganishi: Paulo anawakumbusha hawa waamini kwamba Mungu aliwafanya watu wamataifa na Wayahudi kuwa mwili mmoja kupitia Kristo na msalaba wake. # wamataifa kwa jinsi ya mwili Hii inaongelea juu watu ambao hawakuzaliwa Wayahudi. # msiyotairiwa Watu ambao si Wayahudi hawakutairiwa walipokuwa watoto na hivyo Wayahudi waliwaona hao kama watu wasiomfuata Mungu. # tohara Hili lilikuwa neno lingine linaloelezea juu ya Wayahudi kwa sababu watoto wote wachanga wa kiume walitairiwa walipokuwa na umri wa siku nane. # tohara ya mwili Kutahiriwa kulifanywa juu ya miili ya watoto wadogo wa kiume. # watu wa Israel "jamii ya watu wa Israel" # wageni kwa agano la ahadi Tafsiri mbadala: "hamkujua ahadi za agano la Mungu"