sw_tn/ecc/11/09.md

24 lines
680 B
Markdown

# Furahia kijana, katika ujana wako, na moyo wako ufurahie siku za ujana wako
Misemo hii miwili inamaanisha kitu kimoja na imeunganishwa kwa ajili ya msisitizo.
# moyo wako ufurahie
Hapa neno "moyo" inamaanisha hisia. "uwe na furaha"
# Fuatilia yale mema ya moyo wako
Hapa neno "moyo" inaweza kumaanisha akili au hisia. "Fuatilia vitu vizuri unavyotamani" au "Fuatilia vitu vyema ulivyokusudia kufuatilia"
# chochote kilicho mbele ya macho yako
"Chochote unachoona na kutamani" au "chochote unachoona kinafaa"
# Mungu atakuleta hukumuni kwa ajili ya vitu hivi vyote
"Mungu atakuwajibisha kwa matendo yako yote"
# Ondoa hasira kutoka moyoni mwako
"Kataa kuwa na hasira"