# Furahia kijana, katika ujana wako, na moyo wako ufurahie siku za ujana wako Misemo hii miwili inamaanisha kitu kimoja na imeunganishwa kwa ajili ya msisitizo. # moyo wako ufurahie Hapa neno "moyo" inamaanisha hisia. "uwe na furaha" # Fuatilia yale mema ya moyo wako Hapa neno "moyo" inaweza kumaanisha akili au hisia. "Fuatilia vitu vizuri unavyotamani" au "Fuatilia vitu vyema ulivyokusudia kufuatilia" # chochote kilicho mbele ya macho yako "Chochote unachoona na kutamani" au "chochote unachoona kinafaa" # Mungu atakuleta hukumuni kwa ajili ya vitu hivi vyote "Mungu atakuwajibisha kwa matendo yako yote" # Ondoa hasira kutoka moyoni mwako "Kataa kuwa na hasira"