sw_tn/deu/22/20.md

1.1 KiB

Taarifa ya Jumla:

Musa anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.

Ila kama jambo hili ni la kweli

"Lakini kama ni kweli" au "Lakini kama kile ambacho mwanamume anasema ni kweli"

kwamba ushahidi wa bikira ya binti haukupatikana kwa binti

Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ya kwamba mwanamume hakupata ushahidi ya kwamba binti alikuwa bikira"

ushahidi wa bikra

Nomino zinazojitegemea za "ushahidi" na "bikira" zinaweza kutafsiriwa kama misemo ya vitenzi. "kitu kinachothibitisha ya kwamba binti alikuwa bikira"

basi wanapaswa kumpeleka binti

"kisha wazee wanapaswa kumtoa binti nje"

kumpiga kwa mawe hadi afe

"kutupa mawe kwake mpaka afe"

kwa sababu amefanya jambo la aibu katika Israeli

"kwa sababu amefanya jambo la aibu katika Israeli"

kwa kutenda kama kahaba chini ya nyumba ya baba yake

"kutenda kama kahaba angali akiishi katika nyumba ya baba yake"

mtakuwa mmeondoa uovu

Kivumishi "uovu" kinaweza kutafsiriwa kama msemo wa nomino. "unapaswa kutoa miongoni mwa Waisraeli mtu ambaye anafanya jambo hili ovu" au "unapaswa kumuua mtu huyu muovu"