# Taarifa ya Jumla: Musa anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli. # Ila kama jambo hili ni la kweli "Lakini kama ni kweli" au "Lakini kama kile ambacho mwanamume anasema ni kweli" # kwamba ushahidi wa bikira ya binti haukupatikana kwa binti Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "ya kwamba mwanamume hakupata ushahidi ya kwamba binti alikuwa bikira" # ushahidi wa bikra Nomino zinazojitegemea za "ushahidi" na "bikira" zinaweza kutafsiriwa kama misemo ya vitenzi. "kitu kinachothibitisha ya kwamba binti alikuwa bikira" # basi wanapaswa kumpeleka binti "kisha wazee wanapaswa kumtoa binti nje" # kumpiga kwa mawe hadi afe "kutupa mawe kwake mpaka afe" # kwa sababu amefanya jambo la aibu katika Israeli "kwa sababu amefanya jambo la aibu katika Israeli" # kwa kutenda kama kahaba chini ya nyumba ya baba yake "kutenda kama kahaba angali akiishi katika nyumba ya baba yake" # mtakuwa mmeondoa uovu Kivumishi "uovu" kinaweza kutafsiriwa kama msemo wa nomino. "unapaswa kutoa miongoni mwa Waisraeli mtu ambaye anafanya jambo hili ovu" au "unapaswa kumuua mtu huyu muovu"