sw_tn/dan/10/07.md

784 B

Hivyo niliachwa peke yangu

"Hakuna yeyote aliyekuwa pamoja nami, na niliona"

mwonekano wangu wa kung'aa ulibadilika na kuwa mwonekano wa uharibifu

Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "mwonekano wangu unaong'aa ulibadilika kuwa katika mwonekano ulioharibiwa"

mwonekano wangu wa kung'aa

Hii inaelezea juu ya uso wa mtu fulani ambaye ana afya nzuri.

Mwonekano ulioharibiwa

Uso mbaya, usio na afya na wa kikatili unasemwa kana kwamba ni jengo.

Nilisikia maneno yake

Hii ina maana kwamba mtu fulani alikuwa anazungumza katika maono. Hii yaweza kuwekwa wazi. "Nilisikia maneno ya mtu aliyekuwa anaongea"

nilianguka kifudifudi na kupata usingizi mzito

Danieli aliogopeshwa na kile alichokiona na ya kwamba huenda alilala chini ardhini, mahali ambapo alizimia.