# Hivyo niliachwa peke yangu "Hakuna yeyote aliyekuwa pamoja nami, na niliona" # mwonekano wangu wa kung'aa ulibadilika na kuwa mwonekano wa uharibifu Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "mwonekano wangu unaong'aa ulibadilika kuwa katika mwonekano ulioharibiwa" # mwonekano wangu wa kung'aa Hii inaelezea juu ya uso wa mtu fulani ambaye ana afya nzuri. # Mwonekano ulioharibiwa Uso mbaya, usio na afya na wa kikatili unasemwa kana kwamba ni jengo. # Nilisikia maneno yake Hii ina maana kwamba mtu fulani alikuwa anazungumza katika maono. Hii yaweza kuwekwa wazi. "Nilisikia maneno ya mtu aliyekuwa anaongea" # nilianguka kifudifudi na kupata usingizi mzito Danieli aliogopeshwa na kile alichokiona na ya kwamba huenda alilala chini ardhini, mahali ambapo alizimia.