sw_tn/dan/04/35.md

812 B

Maelezo ya jumla

Katika mistari ya 34-37 Nebukadneza anaongelea katika nafsi ya kwanza katika kueleza jibu lake kwa Mungu.

Wenyeji wote wa duniani huhesabiwa na yeye kuwa bure

Sentensi hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Huwahesabu wakaaji wote wa duniani kuwa si kitu"

Wenyeji wote wa duniani

"watu wote katika dunia"

jeshi la mbinguni

"jeshi la malaika huko mbinguni"

hufanya lolote limpendezalo

"lolote linalotimiza kusudi lake" au kila kitu anachotaka kufanya"

Hakuna hata mmoja awezaye kumzuia

Itakuwa na msaada kuongeza maelezo ya ziada. "Hakuna hata mmoja awezaye kumzuia kufanya kile alichoamua kufanya"

Hakuna hata mmoja awezaye kumwambia, "Mbona umefanya hivi?"

Hii yaweza kuelezeka kwa kutumia nukuru isiyo ya moja kwa moja. "Hakuna awezaye kumwuliza kile anachofanya"