# Maelezo ya jumla Katika mistari ya 34-37 Nebukadneza anaongelea katika nafsi ya kwanza katika kueleza jibu lake kwa Mungu. # Wenyeji wote wa duniani huhesabiwa na yeye kuwa bure Sentensi hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Huwahesabu wakaaji wote wa duniani kuwa si kitu" # Wenyeji wote wa duniani "watu wote katika dunia" # jeshi la mbinguni "jeshi la malaika huko mbinguni" # hufanya lolote limpendezalo "lolote linalotimiza kusudi lake" au kila kitu anachotaka kufanya" # Hakuna hata mmoja awezaye kumzuia Itakuwa na msaada kuongeza maelezo ya ziada. "Hakuna hata mmoja awezaye kumzuia kufanya kile alichoamua kufanya" # Hakuna hata mmoja awezaye kumwambia, "Mbona umefanya hivi?" Hii yaweza kuelezeka kwa kutumia nukuru isiyo ya moja kwa moja. "Hakuna awezaye kumwuliza kile anachofanya"