sw_tn/col/02/01.md

48 lines
1.6 KiB
Markdown

# Sentensi unganishi:
Paulo anaendelea kuwatia moyo walioamini katika Kolosai na Laodekia wapate kuelewa kuwa Kristo ni Mungu na anaishi ndani ya walioamini ili wapate kuishi sawasawa na walivyompokea.
# Ni mapambano ya jinsi gani niliyopitia kwa ajili yenu
Paulo amefanya bidii nyingi katika kuendeleza usafi wao na uelewa wa injili.
# Wale waliopo Laodekia
Huu ulikuwa mji karibu sana na Kolosai ambamo pia kulikuwa na kanisa ambalo Paulo alikuwa akiliombea.
# kama ambavyo wengi hawajaniona uso wangu katika mwili
"wengi ambao mimi binafsi sijawaona" au "wengi ambao sijaonana nao uso kwa uso"
# kwamba mioyo yao
"kwamba mioyo ya wote walioamini ambao hawakuwa wamemuona Paulo"
# walioletwa pamoja
waliowekwa pamoja katika ushirika halisi wa karibu
# utajiri wote wa uhakika kamili wa maarifa
Paulo nazungumza na mtu anauhakika kamili kwamba habari njema ni kweli ingawa huyo mtu alikuwa tajiri katika mwili huu.
# siri ya Mungu ya kweli ya Mungu
Huu ufahamu ambao unaweza kufunuliwa na Mungu peke yake.
# ambaye ni, Kristi
Yesu Kristo ndiye siri ya kweli iliyofunuliwa na Mungu.
# Katika yeye hazina za hekima na maarifa zilizofichika
Kristo pekee ndiye awezaye kufunua hekima ya kweli ya Mungu na maarifa. "Mungu ameficha hazina zote za hekima na maarifa katika Kristo"
# hazina ya hekima na ufahamu
Kimsingi Paulo anazungumzia hekima na maarifa ya Mungu kana kwamba vilikuwa malighafi ya utajiri.
# hekima na ujuzi
Kimsingi haya maneno hapa haya maneno yanamaanisha vitu viwili. Paulo ametumia yote pomaja kusisitiza kwamba ufahamu wote wa kiroho unatokana na Kristo.