sw_tn/col/02/01.md

1.6 KiB

Sentensi unganishi:

Paulo anaendelea kuwatia moyo walioamini katika Kolosai na Laodekia wapate kuelewa kuwa Kristo ni Mungu na anaishi ndani ya walioamini ili wapate kuishi sawasawa na walivyompokea.

Ni mapambano ya jinsi gani niliyopitia kwa ajili yenu

Paulo amefanya bidii nyingi katika kuendeleza usafi wao na uelewa wa injili.

Wale waliopo Laodekia

Huu ulikuwa mji karibu sana na Kolosai ambamo pia kulikuwa na kanisa ambalo Paulo alikuwa akiliombea.

kama ambavyo wengi hawajaniona uso wangu katika mwili

"wengi ambao mimi binafsi sijawaona" au "wengi ambao sijaonana nao uso kwa uso"

kwamba mioyo yao

"kwamba mioyo ya wote walioamini ambao hawakuwa wamemuona Paulo"

walioletwa pamoja

waliowekwa pamoja katika ushirika halisi wa karibu

utajiri wote wa uhakika kamili wa maarifa

Paulo nazungumza na mtu anauhakika kamili kwamba habari njema ni kweli ingawa huyo mtu alikuwa tajiri katika mwili huu.

siri ya Mungu ya kweli ya Mungu

Huu ufahamu ambao unaweza kufunuliwa na Mungu peke yake.

ambaye ni, Kristi

Yesu Kristo ndiye siri ya kweli iliyofunuliwa na Mungu.

Katika yeye hazina za hekima na maarifa zilizofichika

Kristo pekee ndiye awezaye kufunua hekima ya kweli ya Mungu na maarifa. "Mungu ameficha hazina zote za hekima na maarifa katika Kristo"

hazina ya hekima na ufahamu

Kimsingi Paulo anazungumzia hekima na maarifa ya Mungu kana kwamba vilikuwa malighafi ya utajiri.

hekima na ujuzi

Kimsingi haya maneno hapa haya maneno yanamaanisha vitu viwili. Paulo ametumia yote pomaja kusisitiza kwamba ufahamu wote wa kiroho unatokana na Kristo.