sw_tn/act/14/14.md

36 lines
933 B
Markdown

# mitume, Barnaba na Paulo
Inawezekana Luka anatumia "mtume" katika hali ya ujumla ya "yule ambaye ametumwa."
# walichana nguo zao
Hili ni tendo la ishara kuonesha kuwa walihuzunishwa na kukasirishwa kwamba kundi lilitaka kuwatolea wao sadaka.
# Watu, kwa nini mnafanya hivi vitu?
Barnaba na Paulo wanawakaripia watu kwa kujaribu kuwatolea sadaka. "watu, hampaswi kutuabudu!"
# Sisi pia ni binadamu wenye hisia kama nyie
Kwa kauli hii, Baranaba na Paulo wanasema kuwa wao sio miungu. "Sisi ni binadamu tu kama nyie.. Sisi sio miungu!"
# wenye hisia sawa na nyie
"kama nyie kwa kila hali"
# mgeukieni Mungu aliye hai kutoka kwa vitu hivi visivyo na maana
"acheni kuabudu miungu ambayo haiwezi kuwasaidia, na badala yake anzeni kumuabudu Mungu aliye hai"
# Mungu aliye hai
"Mungu ambaye kweli yupo" au "Mungu anayeishi"
# Siku za nyuma
"katika nyakati za zamani" au "Hadi sasa"
# kutembea katika
"kuishi kulingana na"