sw_tn/act/12/13.md

52 lines
1.2 KiB
Markdown

# Maelezo ya jumla
Maelezo haya yanawataja binti Rhoda pamoja na wote waliokuwa wakiomba mle chumbani.
# Alibisha mlangoni
"Petro alibisha mlangoni" Alizidi kugongagonga kama ilivyokuwa desturi ya Wayahudi ili kuruhusu waliopo kujua kuwa wametembelewa.
# kwenye mlango wa kizuizi
"Katika mlango wa nje" au "Katika mlango wa kuingilia kutoka barabarani hadi kwenye yadi ya nyumba"
# Akaja kufungua
"Alikuja getini kuuliza ni nani aliyekuwa anabisha hodi"
# Kwa furaha
"Kwa vile alijawa na furaha" au "Furaha kupita kiasi"
# Alishindwa kuufungua mlango
"Hakuweza kuufungua mlango" au "Alisahau kufungua mlango"
# akakimbia ndani ya chumba
"Alikwenda mbio kwenye chumba cha nyumba ile"
# na kuwajulisha
liwajulisha au "Alisema"
# Petro amesimama mbele ya Mlango
"Amesimama nje mbele ya mlango"
# Wewe ni mwendawazimu
Watu siyo tu hawakumwamini, bali walimkemea pia kwa kusema maneno ya kipuuzi.
# lakini alikazia kuwa ni kweli
"Alisisitiza kusema alichowaambia kilikuwa cha kweli"
# Wakamwambia
"Walimwambia"
# Ni malaika wake
"KIle ulichokiona ni malaika wa Petro" Wayahudi waliamini kuwa na malaika mlinzi na inawezekana walifikiri kwa Petro hivyo, kuwa malaika wa Petro alikuwa amekuja kwao.