# Maelezo ya jumla Maelezo haya yanawataja binti Rhoda pamoja na wote waliokuwa wakiomba mle chumbani. # Alibisha mlangoni "Petro alibisha mlangoni" Alizidi kugongagonga kama ilivyokuwa desturi ya Wayahudi ili kuruhusu waliopo kujua kuwa wametembelewa. # kwenye mlango wa kizuizi "Katika mlango wa nje" au "Katika mlango wa kuingilia kutoka barabarani hadi kwenye yadi ya nyumba" # Akaja kufungua "Alikuja getini kuuliza ni nani aliyekuwa anabisha hodi" # Kwa furaha "Kwa vile alijawa na furaha" au "Furaha kupita kiasi" # Alishindwa kuufungua mlango "Hakuweza kuufungua mlango" au "Alisahau kufungua mlango" # akakimbia ndani ya chumba "Alikwenda mbio kwenye chumba cha nyumba ile" # na kuwajulisha liwajulisha au "Alisema" # Petro amesimama mbele ya Mlango "Amesimama nje mbele ya mlango" # Wewe ni mwendawazimu Watu siyo tu hawakumwamini, bali walimkemea pia kwa kusema maneno ya kipuuzi. # lakini alikazia kuwa ni kweli "Alisisitiza kusema alichowaambia kilikuwa cha kweli" # Wakamwambia "Walimwambia" # Ni malaika wake "KIle ulichokiona ni malaika wa Petro" Wayahudi waliamini kuwa na malaika mlinzi na inawezekana walifikiri kwa Petro hivyo, kuwa malaika wa Petro alikuwa amekuja kwao.