sw_tn/3jn/01/09.md

890 B

Maelezo ya jumla

Neno "sisi" linamwelezea Yohana na wele waliokuwa pamoja naye bila kumjumuisha Gayo.

kusanyiko

Hapa anamtaja Gayo na kundi la waumini wanaokutana pamoja kumwabudu Mungu.

Diotrofe

Alikuwa hapo awali mmoja wa kundi la waumini waliokuwa wakikusanyika

anayependa kuwa wa kwanza miongoni mwao

"Aliyependa kuonekana kuwa wa muhimu sana miongoni mwao" au "ambaye alipenda kujifanya kama vile ni kiongozi wao"

jinsi anavyosema maneno mabaya dhidi yetu

"Jinsi anavyonena mambo mabaya kutuhusu sisi na hakika siyo ya kweli"

yeye mwenyewe

Neno "yeye mwenyewe" linamwelezea Diotrofe aliyekuwa akifanya mambo hayo.

hawapokei ndugu

hataki kuwapokea ndugu waumini"

Hata huwakataza wengine ambao wanatamani kuwakaribisha hao

"Anawazuia wale wanaotaka kuwakaribisha waumini"

na kuwafukuza watoke kwenye kusanyiko.

"Anawalazimisha kutoka kwenye kusanyiko"