# Maelezo ya jumla Neno "sisi" linamwelezea Yohana na wele waliokuwa pamoja naye bila kumjumuisha Gayo. # kusanyiko Hapa anamtaja Gayo na kundi la waumini wanaokutana pamoja kumwabudu Mungu. # Diotrofe Alikuwa hapo awali mmoja wa kundi la waumini waliokuwa wakikusanyika # anayependa kuwa wa kwanza miongoni mwao "Aliyependa kuonekana kuwa wa muhimu sana miongoni mwao" au "ambaye alipenda kujifanya kama vile ni kiongozi wao" # jinsi anavyosema maneno mabaya dhidi yetu "Jinsi anavyonena mambo mabaya kutuhusu sisi na hakika siyo ya kweli" # yeye mwenyewe Neno "yeye mwenyewe" linamwelezea Diotrofe aliyekuwa akifanya mambo hayo. # hawapokei ndugu hataki kuwapokea ndugu waumini" # Hata huwakataza wengine ambao wanatamani kuwakaribisha hao "Anawazuia wale wanaotaka kuwakaribisha waumini" # na kuwafukuza watoke kwenye kusanyiko. "Anawalazimisha kutoka kwenye kusanyiko"