sw_tn/3jn/01/05.md

44 lines
1.2 KiB
Markdown

# Sentensi unganishi
Kusudi la Yohana la kuandika barua hii ilikuwa kumhimiza Gayo kuwa makini katika njia aliyoianza ya kufundisha Biblia; kisha anazungumzia habari za watu wawili, mmoja mwovu na mwingine mwema.
# Maelezo ya Jumla
Hapa neno "sisi" linamtambulisha Yohana na wale waliokuwa pamoja naye na yawezekana linawaunganisha waumini wote.
# Mpendwa
Hapa inatumika kama neno la utambulisho kwa wafuasi waumini.
# Unaenenda kwa uaminifu
"Unatenda kwa uaminifu kwa Mungu" au "Umekuwa mtii kwa Mungu"
# unapowahudumia ndugu na wageni
"Kuhudumia ndugu waumini na wale usiowajua"
# ambao wametoa ushuhuda wa upendo wako mbele ya kanisa.
"Wageni, ambao wamewaambia waumini katika kanisa jinsi mnavyowapenda"
# Unafanya vizuri kuwasafirisha
"Kwa unyenyekevu ninawaomba mpate kuwasafirisha
# Kwa sababu kwa ajili ya Jina, walienda
Hapa Jina linamaanisha Yesu. Walienda kuwaambia watu wengine kuhusu Yesu.
# bila kuchukua kitu chochote
Bila kupokea zawadi au misaada
# wa Mataifa
Hapa watu "wa mataifa" Haimaanishi kuwa ni watu wasio Wayahudi. Inamaanisha watu wasio na tumaini kwa Yesu.
# ili tuwe watenda kazi wenza kwa ajili ya kweli
"Ili kwamba tutashirikiana nao kuutangaza ukweli wa Mungu kwa watu"