sw_tn/3jn/01/05.md

1.2 KiB

Sentensi unganishi

Kusudi la Yohana la kuandika barua hii ilikuwa kumhimiza Gayo kuwa makini katika njia aliyoianza ya kufundisha Biblia; kisha anazungumzia habari za watu wawili, mmoja mwovu na mwingine mwema.

Maelezo ya Jumla

Hapa neno "sisi" linamtambulisha Yohana na wale waliokuwa pamoja naye na yawezekana linawaunganisha waumini wote.

Mpendwa

Hapa inatumika kama neno la utambulisho kwa wafuasi waumini.

Unaenenda kwa uaminifu

"Unatenda kwa uaminifu kwa Mungu" au "Umekuwa mtii kwa Mungu"

unapowahudumia ndugu na wageni

"Kuhudumia ndugu waumini na wale usiowajua"

ambao wametoa ushuhuda wa upendo wako mbele ya kanisa.

"Wageni, ambao wamewaambia waumini katika kanisa jinsi mnavyowapenda"

Unafanya vizuri kuwasafirisha

"Kwa unyenyekevu ninawaomba mpate kuwasafirisha

Kwa sababu kwa ajili ya Jina, walienda

Hapa Jina linamaanisha Yesu. Walienda kuwaambia watu wengine kuhusu Yesu.

bila kuchukua kitu chochote

Bila kupokea zawadi au misaada

wa Mataifa

Hapa watu "wa mataifa" Haimaanishi kuwa ni watu wasio Wayahudi. Inamaanisha watu wasio na tumaini kwa Yesu.

ili tuwe watenda kazi wenza kwa ajili ya kweli

"Ili kwamba tutashirikiana nao kuutangaza ukweli wa Mungu kwa watu"