# Sentensi unganishi Kusudi la Yohana la kuandika barua hii ilikuwa kumhimiza Gayo kuwa makini katika njia aliyoianza ya kufundisha Biblia; kisha anazungumzia habari za watu wawili, mmoja mwovu na mwingine mwema. # Maelezo ya Jumla Hapa neno "sisi" linamtambulisha Yohana na wale waliokuwa pamoja naye na yawezekana linawaunganisha waumini wote. # Mpendwa Hapa inatumika kama neno la utambulisho kwa wafuasi waumini. # Unaenenda kwa uaminifu "Unatenda kwa uaminifu kwa Mungu" au "Umekuwa mtii kwa Mungu" # unapowahudumia ndugu na wageni "Kuhudumia ndugu waumini na wale usiowajua" # ambao wametoa ushuhuda wa upendo wako mbele ya kanisa. "Wageni, ambao wamewaambia waumini katika kanisa jinsi mnavyowapenda" # Unafanya vizuri kuwasafirisha "Kwa unyenyekevu ninawaomba mpate kuwasafirisha # Kwa sababu kwa ajili ya Jina, walienda Hapa Jina linamaanisha Yesu. Walienda kuwaambia watu wengine kuhusu Yesu. # bila kuchukua kitu chochote Bila kupokea zawadi au misaada # wa Mataifa Hapa watu "wa mataifa" Haimaanishi kuwa ni watu wasio Wayahudi. Inamaanisha watu wasio na tumaini kwa Yesu. # ili tuwe watenda kazi wenza kwa ajili ya kweli "Ili kwamba tutashirikiana nao kuutangaza ukweli wa Mungu kwa watu"