sw_tn/2co/06/04.md

1.3 KiB

Habari za Jumla

Wakati Paulo anapotumia neno " sisi", ana maanisha yeye mwenyewe na Timotheo.

Tunajihakiki wenyewe kwa matendo yetu yote, kwamba tu watumishi wa Mungu.

"Tunathibitisha kjwa sisi ni watumishi wa Mungu kwa kila kile tulifanyalo"

Tu watumishi wake katika wingi wa ustahimilivu.... katika kukosa usingizi usiku, katika njaa

Paulo anataja maeneo mbali mbali ya mazingira magumu katika hayo wanathibitisha kuwa ni watumishi wa Mungu.

katika usafi...katika upendo halisi.

Paulo anaorodhesha mambo mbalimbali ya uadilifu ambayo waliyatunza wakati wa mazingira magumu na inathibisha kuwa ni watumishi wa Mungu.

Tu watumishi wake katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu

Kuwekwwakfu kwao kuihubiri injili katika nguvu za Mungu inathibitisha kuwa ni watumishi wa Mungu.

katika neno la kweli

"katika kuhubiri neno la kweli la Mungu"

Tuna silaha ya haki kwa ajili ya mkono wa kuume na wa kushoto

Paulo anazungumza juu ya uadilifu wao kama vile silama wanazozitumia kupigana vita vya kiroho.

Tuna silaha ya haki kwa ajili ya mkono wa kuuume na wa kushoto.

"uadilifu kama silaha yetu " au "uadilifu kama silaha zetu"

kwa mkono wa kuume na wa kushoto

Maana zaweza kuwa hizi: "kuwa kuna silaha katika mkono mmoja na ngao mkono mwingine" au "wamewezeshwa kikamilifu kwa vita , tayari kujilinda na mashambulizi kutoka sehemu yoyote."