# Habari za Jumla Wakati Paulo anapotumia neno " sisi", ana maanisha yeye mwenyewe na Timotheo. # Tunajihakiki wenyewe kwa matendo yetu yote, kwamba tu watumishi wa Mungu. "Tunathibitisha kjwa sisi ni watumishi wa Mungu kwa kila kile tulifanyalo" # Tu watumishi wake katika wingi wa ustahimilivu.... katika kukosa usingizi usiku, katika njaa Paulo anataja maeneo mbali mbali ya mazingira magumu katika hayo wanathibitisha kuwa ni watumishi wa Mungu. # katika usafi...katika upendo halisi. Paulo anaorodhesha mambo mbalimbali ya uadilifu ambayo waliyatunza wakati wa mazingira magumu na inathibisha kuwa ni watumishi wa Mungu. # Tu watumishi wake katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu Kuwekwwakfu kwao kuihubiri injili katika nguvu za Mungu inathibitisha kuwa ni watumishi wa Mungu. # katika neno la kweli "katika kuhubiri neno la kweli la Mungu" # Tuna silaha ya haki kwa ajili ya mkono wa kuume na wa kushoto Paulo anazungumza juu ya uadilifu wao kama vile silama wanazozitumia kupigana vita vya kiroho. # Tuna silaha ya haki kwa ajili ya mkono wa kuuume na wa kushoto. "uadilifu kama silaha yetu " au "uadilifu kama silaha zetu" # kwa mkono wa kuume na wa kushoto Maana zaweza kuwa hizi: "kuwa kuna silaha katika mkono mmoja na ngao mkono mwingine" au "wamewezeshwa kikamilifu kwa vita , tayari kujilinda na mashambulizi kutoka sehemu yoyote."