sw_tn/2co/06/04.md

36 lines
1.3 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Habari za Jumla
Wakati Paulo anapotumia neno " sisi", ana maanisha yeye mwenyewe na Timotheo.
# Tunajihakiki wenyewe kwa matendo yetu yote, kwamba tu watumishi wa Mungu.
"Tunathibitisha kjwa sisi ni watumishi wa Mungu kwa kila kile tulifanyalo"
# Tu watumishi wake katika wingi wa ustahimilivu.... katika kukosa usingizi usiku, katika njaa
Paulo anataja maeneo mbali mbali ya mazingira magumu katika hayo wanathibitisha kuwa ni watumishi wa Mungu.
# katika usafi...katika upendo halisi.
Paulo anaorodhesha mambo mbalimbali ya uadilifu ambayo waliyatunza wakati wa mazingira magumu na inathibisha kuwa ni watumishi wa Mungu.
# Tu watumishi wake katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu
Kuwekwwakfu kwao kuihubiri injili katika nguvu za Mungu inathibitisha kuwa ni watumishi wa Mungu.
# katika neno la kweli
"katika kuhubiri neno la kweli la Mungu"
# Tuna silaha ya haki kwa ajili ya mkono wa kuume na wa kushoto
Paulo anazungumza juu ya uadilifu wao kama vile silama wanazozitumia kupigana vita vya kiroho.
# Tuna silaha ya haki kwa ajili ya mkono wa kuuume na wa kushoto.
"uadilifu kama silaha yetu " au "uadilifu kama silaha zetu"
# kwa mkono wa kuume na wa kushoto
Maana zaweza kuwa hizi: "kuwa kuna silaha katika mkono mmoja na ngao mkono mwingine" au "wamewezeshwa kikamilifu kwa vita , tayari kujilinda na mashambulizi kutoka sehemu yoyote."