sw_tn/2co/01/08.md

1.0 KiB

hatutaki mwe wajinga

Hii inaweza kuelezwa kwa msamiati chanya "tunataka mfahamu"

Tuliteswa sana zaidi ya vile ambavyo tungeweza kuvumilia

Paulo na Timotheo wanaelezea hisia zao za kukata tamaa kama mzigo mzito waliopaswa kuubeba.

Tulikuwa tumekatishwa tamaa kabisa

neno "katishwa tamaa" linaeleza hisia za kuvujwa moyo. Hii inaweza kuelezwa katika muundo wa utendaji. " taabu tulizozipitia zimetukatisha tamaa kabisa" au "Tulikuwa katika kukatishwa tamaa kabisa"

Tulikuwa na hukumu ya kifo juu yetu

Paulo na Timotheo wanalinganisha hisia zao za kuvujwa moyo kama mtu ambaye ametiwa hatiani kufa." " Tulikuwa katika kukata tamaa kama mtu aliyehukumiwa kufa"

lakini badala yake katika Mungu

Maneno "weka tumaini letu" yameachwa katika sentensi hii. "lakini badala yake, weka tumaini letu katika Mungu"

anaye wafufua wafu

"anaye waleta wafu kurudi katika uhai tena"

maafa ya mauti

Paulo na Timotheo wanafananisha hisia yao ya kukata tamaa na maafa ya mauti au hatari ya kutisha. (UDB) AT: "kukata tamaa."