sw_tn/rev/02/10.md

28 lines
989 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Ibilisi anataka kuwatupa baadhi yenu gerezani
"Ibilisi atasababisha hivi punde wengine wawaweke baadhi yenu gerezani"
# Iweni waaminifu hadi kufa
"Kuweni waaminifu kwangu hata kama watawaua". Matumizi ya neno "hadi" haimanishi kuwa uache kuwa mwaminifu wakati wa kifo.
# taji
"taji la ushindi." Hili lilikua shada ambalo asili yake ilikua ya matawi ya mizeituni au majani ya laurusi ambayo yaliweka kwenye kichwa cha mwanariadha mshindi.
# taji la uzima
Maana zinazowezekana ni 1)"taji linaloonesha kuwa nimekupa uzima wa milele" au 2)"uzima wa kweli kama dhawabu kama taji la mshindi"
# Mwenye sikio asikie
Kuwa tayari kusikiliza inazungumziwa kama kuwa na sikio. "Acha ambaye yuko tayari kusikiliza asiklize" au "kama uko tayari kusikiliza, sikiliza"
# Yeye ashindaye
hii humaanisha mtu yeyote atakayeshinda. "yeyote atakayekataa uovu" au "kwa wale ambao hawatakubali kufanya uovu"
# hatapata madhara ya mauti ya pili
"hatapitia kifo cha pili" au "hatakufa mara ya pili"