# Ibilisi anataka kuwatupa baadhi yenu gerezani "Ibilisi atasababisha hivi punde wengine wawaweke baadhi yenu gerezani" # Iweni waaminifu hadi kufa "Kuweni waaminifu kwangu hata kama watawaua". Matumizi ya neno "hadi" haimanishi kuwa uache kuwa mwaminifu wakati wa kifo. # taji "taji la ushindi." Hili lilikua shada ambalo asili yake ilikua ya matawi ya mizeituni au majani ya laurusi ambayo yaliweka kwenye kichwa cha mwanariadha mshindi. # taji la uzima Maana zinazowezekana ni 1)"taji linaloonesha kuwa nimekupa uzima wa milele" au 2)"uzima wa kweli kama dhawabu kama taji la mshindi" # Mwenye sikio asikie Kuwa tayari kusikiliza inazungumziwa kama kuwa na sikio. "Acha ambaye yuko tayari kusikiliza asiklize" au "kama uko tayari kusikiliza, sikiliza" # Yeye ashindaye hii humaanisha mtu yeyote atakayeshinda. "yeyote atakayekataa uovu" au "kwa wale ambao hawatakubali kufanya uovu" # hatapata madhara ya mauti ya pili "hatapitia kifo cha pili" au "hatakufa mara ya pili"