sw_tn/mat/10/14.md

40 lines
1.1 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Sentensi unganishi
Yesu anaendelea kuwaelekeza wanafunzi wake cha kufanya watakapoenda kuhubiri
# Na kwa wale wasiowapokea au kusikiliza
"Ikiwa hakuna watu watakaowakaribisha au kuwasikia katika mji huo"
# ninyi ... yenu
Hivi ni viwakilishi vya wingi ambavyo vinamaanisha mitume kumi na mbili
# kusikiliza maneno yenu
Hapa "maneno" inamaanisjha kile ambacho wanafunzi wa Yesu watasema. "kusikiliza ujumbe wenu" au "kusikiliza kile mnachotaka kusema"
# mji
Unaweza kutafsiri kama ulivyofanya kwa njia hiyo hiyo
# jipanguseni mavumbi ya mguuni
"jipanguseni mavumbi y a miguu yenu mnapoondoka." Hii ni ishara inayoonesha kuwa Mungu amaewakataa watu wa mji au nyumba hiyo.
# kweli nawaambia
"Nawaambia ukweli." Kirai hiki kinaongeza msisitizo kwa kile ambacho Yesu atasema baadaye.
# itakuwa zaidi ya kuvumilia
"mateso yatakuwa machache"
# mji wa Sodoma na Gomora
Hii inamaanisha watu walioishi Sodoma na Gomora."watu ambao waliishi katika miji ya Sodoma na Gomora"
# mji huo
Hii inamaanisha watu katika mji ambao hawakutaka kuwapokea mitume au kusikiliza ujumbe wao. "Watu wa mji huo ambao hawakuwapokea"