# Sentensi unganishi Yesu anaendelea kuwaelekeza wanafunzi wake cha kufanya watakapoenda kuhubiri # Na kwa wale wasiowapokea au kusikiliza "Ikiwa hakuna watu watakaowakaribisha au kuwasikia katika mji huo" # ninyi ... yenu Hivi ni viwakilishi vya wingi ambavyo vinamaanisha mitume kumi na mbili # kusikiliza maneno yenu Hapa "maneno" inamaanisjha kile ambacho wanafunzi wa Yesu watasema. "kusikiliza ujumbe wenu" au "kusikiliza kile mnachotaka kusema" # mji Unaweza kutafsiri kama ulivyofanya kwa njia hiyo hiyo # jipanguseni mavumbi ya mguuni "jipanguseni mavumbi y a miguu yenu mnapoondoka." Hii ni ishara inayoonesha kuwa Mungu amaewakataa watu wa mji au nyumba hiyo. # kweli nawaambia "Nawaambia ukweli." Kirai hiki kinaongeza msisitizo kwa kile ambacho Yesu atasema baadaye. # itakuwa zaidi ya kuvumilia "mateso yatakuwa machache" # mji wa Sodoma na Gomora Hii inamaanisha watu walioishi Sodoma na Gomora."watu ambao waliishi katika miji ya Sodoma na Gomora" # mji huo Hii inamaanisha watu katika mji ambao hawakutaka kuwapokea mitume au kusikiliza ujumbe wao. "Watu wa mji huo ambao hawakuwapokea"