sw_tn/mat/02/17.md

32 lines
1.0 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Taarifa kwa ujumla:
Mwandishi amnukuu nabii Yeremia kuonesha kwamba kifo cha watoto wote wa kiume katika mkoa wa Bethlehemu kilikuwa kwa mujibu wa Maandiko.
# Kisha ilitimizwa
Hii inaweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "Hii ilitimizwa" au "matendo ya Herode yalitimiza."
# kile kilicho kuwa kimenenwa kwa njia ya nabii Yeremia
Hii inaweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "kile Bwana alikinena hapo zamani kwa njia ya nabii Yeremia"
# Sauti ilisikika...hawakuwapo
Mathayo anamnukuu nabii Yeremia.
# Sauti ilisikika
Hii inaweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "Watu walisikia sauti" au "kulikuwa na sauti kubwa."
# Raheli awalilia watoto wake
Raheli aliishi miaka mingi kabla ya wakati huu. Unabii huu huonesha Raheli, ambaye amekufa, akiwalilia wazaliwa wake.
# alikataa kufarijiwa
Hii inaweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "hakuna yeyote angeweza kumfariji"
# kwa sababu hawapo tena
kwa sababu watoto walikuwa wametoweka na kamwe hawatarudi." Hapa "hawapo tena" ni njia laini ya kusema wamekufa. "kwa sababu walikuwa wamekufa"