# Taarifa kwa ujumla: Mwandishi amnukuu nabii Yeremia kuonesha kwamba kifo cha watoto wote wa kiume katika mkoa wa Bethlehemu kilikuwa kwa mujibu wa Maandiko. # Kisha ilitimizwa Hii inaweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "Hii ilitimizwa" au "matendo ya Herode yalitimiza." # kile kilicho kuwa kimenenwa kwa njia ya nabii Yeremia Hii inaweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "kile Bwana alikinena hapo zamani kwa njia ya nabii Yeremia" # Sauti ilisikika...hawakuwapo Mathayo anamnukuu nabii Yeremia. # Sauti ilisikika Hii inaweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "Watu walisikia sauti" au "kulikuwa na sauti kubwa." # Raheli awalilia watoto wake Raheli aliishi miaka mingi kabla ya wakati huu. Unabii huu huonesha Raheli, ambaye amekufa, akiwalilia wazaliwa wake. # alikataa kufarijiwa Hii inaweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "hakuna yeyote angeweza kumfariji" # kwa sababu hawapo tena kwa sababu watoto walikuwa wametoweka na kamwe hawatarudi." Hapa "hawapo tena" ni njia laini ya kusema wamekufa. "kwa sababu walikuwa wamekufa"