forked from WA-Catalog/sw_tn
36 lines
1.1 KiB
Markdown
36 lines
1.1 KiB
Markdown
|
# kuanzia sasa
|
||
|
|
||
|
"kuanzia siku hii" au "kuanzia kutoka leo"
|
||
|
|
||
|
# Mwana wa Adamu
|
||
|
|
||
|
Yesu alitumia sentensi hii kumaanisha Kristo. Alimaanisha kwamba alikuwa akijiongelea mwenyewe, lakini wazee iliwalazimu kuuliza kuona kama hivyo ndivyo kweli alikuwa akisema.
|
||
|
|
||
|
# amekaa mkono wa kuume wa nguvu ya Mungu
|
||
|
|
||
|
Wayahudi walielewa kwamba hakuna hata mmoja ambaye angeweza kukaa pale.Waliiona hii ni sawa na kusema "atakuwa na Mungu kama Mungu."
|
||
|
|
||
|
# nguvu ya Mungu
|
||
|
|
||
|
"Mungu mwenye nguvu zote." Hapa "nguvu" inamaanisha mamlaka yake kuu.
|
||
|
|
||
|
# Kwa hiyo wewe ni Mwana wa Mungu?
|
||
|
|
||
|
Baraza lilimhukumu Yesu kusulubiwa kwa sababu alijithibitishia kwamba yeye alikuwa "Mwana wa Mungu," akijua Baraza litamhukumu kifo.
|
||
|
|
||
|
# Mwana wa Mungu
|
||
|
|
||
|
Hiki ni cheo muhimu kwa Yesu.
|
||
|
|
||
|
# Ninyi mmesema mimi ndiye
|
||
|
|
||
|
"Ndiyo, ni kama mlivyosema"
|
||
|
|
||
|
# Kwanini bado tunahitaji tena ushahidi?
|
||
|
|
||
|
Walitumia swali kwa kuweka msisitizo. Tafsiri mbadala: "Hatuna haja tena ya kuwa na ushahidi!"
|
||
|
|
||
|
# tumesikia kutoka katika kinywa chake mwenyewe
|
||
|
|
||
|
Tafsiri mbadala: "tumesikia moja kwa moja kutoka kwake kwamba anaamini yeye ni Mwana wa Mungu"
|