# kuanzia sasa "kuanzia siku hii" au "kuanzia kutoka leo" # Mwana wa Adamu Yesu alitumia sentensi hii kumaanisha Kristo. Alimaanisha kwamba alikuwa akijiongelea mwenyewe, lakini wazee iliwalazimu kuuliza kuona kama hivyo ndivyo kweli alikuwa akisema. # amekaa mkono wa kuume wa nguvu ya Mungu Wayahudi walielewa kwamba hakuna hata mmoja ambaye angeweza kukaa pale.Waliiona hii ni sawa na kusema "atakuwa na Mungu kama Mungu." # nguvu ya Mungu "Mungu mwenye nguvu zote." Hapa "nguvu" inamaanisha mamlaka yake kuu. # Kwa hiyo wewe ni Mwana wa Mungu? Baraza lilimhukumu Yesu kusulubiwa kwa sababu alijithibitishia kwamba yeye alikuwa "Mwana wa Mungu," akijua Baraza litamhukumu kifo. # Mwana wa Mungu Hiki ni cheo muhimu kwa Yesu. # Ninyi mmesema mimi ndiye "Ndiyo, ni kama mlivyosema" # Kwanini bado tunahitaji tena ushahidi? Walitumia swali kwa kuweka msisitizo. Tafsiri mbadala: "Hatuna haja tena ya kuwa na ushahidi!" # tumesikia kutoka katika kinywa chake mwenyewe Tafsiri mbadala: "tumesikia moja kwa moja kutoka kwake kwamba anaamini yeye ni Mwana wa Mungu"