sw_tn/act/18/24.md

44 lines
1.2 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Sentensi unganishi
Luka anaelezea kile kilichotokea katika Mji wa Efeso wakiwa na Prisila na Akwira
# Taarifa ya Jumla
Apolo anatambulishwa kwenye hadithi. Mistari ya 24 na 25 inatoa habari kumuhusu yeye.
# Mmoja wa Wayahudi aitwaye Apolo
Hapa Luka anaanza kuelezea habari ya mtu mpya.
# Mzaliwa wa Alexandra
"Mtu ambaye alizaliwa katika mji wa Alexandria". Hii inaweza kuwa ni miji ya 1) "Alexandria huko Misiri katika mwambao wa kaskasini. " au 2) Alexandra huko Asia katika mwambao wa magharibi."
# ufasaha katika kuongea
"mwongeaji mzuri"
# mwenye uwezo katika maandiko
"Alikuwa anayafahamu vema maandiko. Alikuwa anauelewa mzuri wa maandiko ya Agano la Kale.
# Apolo alikuwa ameelimishwa vema katika mafundisho ya Bwana.
"Baadhi ya waumini walikuwa wamemfundisha Apolo namna Bwana Yesu alivyokuwa anataka watu wapate kuishi.
# Alikuwa na bidii katika roho
Neno "roho" linamtambulisha Apolo kama mtu aliyekuwa mwenye nia thabiti ya roho.
# ubatizo wa Yohana
"Ubatizo ambao Yohana alifanya" Huu ni ulinganisho wa ubatizo wa Yohana ambao ulikuwa wa maji na ubatizo wa Yesu ambao ulikuwa wa Roho Mtakatifu.
# njia za Mungu
Namna vile anawataka watu waishi.
# kwa usahihi
"kwa undani zaidi "