# Sentensi unganishi Luka anaelezea kile kilichotokea katika Mji wa Efeso wakiwa na Prisila na Akwira # Taarifa ya Jumla Apolo anatambulishwa kwenye hadithi. Mistari ya 24 na 25 inatoa habari kumuhusu yeye. # Mmoja wa Wayahudi aitwaye Apolo Hapa Luka anaanza kuelezea habari ya mtu mpya. # Mzaliwa wa Alexandra "Mtu ambaye alizaliwa katika mji wa Alexandria". Hii inaweza kuwa ni miji ya 1) "Alexandria huko Misiri katika mwambao wa kaskasini. " au 2) Alexandra huko Asia katika mwambao wa magharibi." # ufasaha katika kuongea "mwongeaji mzuri" # mwenye uwezo katika maandiko "Alikuwa anayafahamu vema maandiko. Alikuwa anauelewa mzuri wa maandiko ya Agano la Kale. # Apolo alikuwa ameelimishwa vema katika mafundisho ya Bwana. "Baadhi ya waumini walikuwa wamemfundisha Apolo namna Bwana Yesu alivyokuwa anataka watu wapate kuishi. # Alikuwa na bidii katika roho Neno "roho" linamtambulisha Apolo kama mtu aliyekuwa mwenye nia thabiti ya roho. # ubatizo wa Yohana "Ubatizo ambao Yohana alifanya" Huu ni ulinganisho wa ubatizo wa Yohana ambao ulikuwa wa maji na ubatizo wa Yesu ambao ulikuwa wa Roho Mtakatifu. # njia za Mungu Namna vile anawataka watu waishi. # kwa usahihi "kwa undani zaidi "